Ujumbe wa Zari baada ya Hamisa Mobeto kupiga Picha na Videographer wa Diamond.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 12 February 2018

Ujumbe wa Zari baada ya Hamisa Mobeto kupiga Picha na Videographer wa Diamond..

Baada ya muimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto kufikishana Mahakamani wiki iliyopita inadaiwa kuwa mambo yao yapo sawa kwa sasa na wamemaliza tofauti zao, hiyo ni baada ya kusambaa kwa picha za official videographer wa Diamond Platnumz ambaye ni Lukamba kusambaa kwa picha mtandaoni akiwa na Hamisa.

Kitendo cha Lukamba kuonekana kumfanyia photoshoot Hamisa kimeanza kuhusishwa kuwa Diamond na Hamisa wapo sawa kwa sasa ndio maana Lukamba ameonekana akifanya kazi za Hamisa ambaye ni mzazi mwenza na boss wake Diamond Platnumz.

Baada ya muda kupita baada ya picha ya Hamisa na Lukamba kusambaa mtandaoni Zari alipost ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa instagram story na kuandika “Nafukuzana na pesa sio binadamu” ujumbe ambao unadaiwa kuwa amepost baada ya kuona picha ya Lukamba na Hamisa wakiwa pamoja kitu ambacho kinadaiwa kuzidi kuyumbisha penzi na Zari na Diamond na indaiwa kuwa bado hawapo sawa kwa sasa.

No comments:

Post a Comment