Mimi Mars:Hizi ndo sifa za Mwanaume ninaye muhitaji - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 4 February 2018

Mimi Mars:Hizi ndo sifa za Mwanaume ninaye muhitaji

Msanii ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya 'Sitamani' chini ya Mdee Music, Mimi Mars amefunguka na kudai endapo atahitaji kuingia katika mahusiano kwa mara nyingine tena basi anataka kuwa na mwanaume mwenye kujielewa na kujitambua.

Mimi amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza baada ya kuulizwa ni kigezo gani huwa anaangalia pindi anapotaka kuwa na mwanaume katika mahusiano yake.

"Awe mtu anajielewa na kujitambua, awe na pesa lakini sio lazima kwa sana maana mimi mwenyewe sasa hivi nimeanza kupata 'mkwanja' kwa hiyo namshukuru Mwenyezi Mungu,' You know its good' vitu viwili vitatu naweza kujifanyia mwenyewe", alisema Mimi Mars.

Pamoja na hayo, Mimi Mars aliendelea kwa kusisitizia baadhi ya mambo kwamba "sana sana awe mtu anajielewa na kuweza kunisaidia hata mimi kunipa changamko katika akili yangu. Ila sitaki mtu ambae yupo katika sekta ambayo mimi nipo ili tuwe na kitu tofauti cha kuongelea"

Kwa upande mwingine, Mimi Mars amesema anatamani siku moja naye aje kuolewa ili aweze kuwa na familia yake pamoja na watoto.

No comments:

Post a Comment