Hii Kali ! Mbwa ageuka kuwa binadamu... - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 24 February 2018

Hii Kali ! Mbwa ageuka kuwa binadamu...

Wananchi wa kijiji cha Mpanda Kata ya Nyimbili  wilayani Mbozi mkoani Songwe wameshikwa na taharuki baada ya mbwa aliyewasumbua kwa siku nyingi kwa matukio ya uhalifu hasa kwa kukamata kuku kijijini hapo kugeuka na kuwa binadamu na kuanza kuongea.

 Afisa Mtendaji wa kijiji hicho amethibitisha tukio hilo kutokea na kuongeza kuwa wamekumbwa natahauki kubwa kuona kitu cha ajabu binadamu kujibadilisha kuwa mbwa na kuanza kufanya uhalifu kitu ambacho kimewashitua wengi. Inadaiwa mbwa huyo kwa siku alikuwa anakamata kuku kuanzia watatu mpaka wa tano.

Mmoja wa wamashuhuda wa tukio hilo alisimulia kuwa "Kuku walianza kupotea muda mrefu kwa hiyo tulichukua jukumu la kumtaarifa Afisa Mtendaji kwamba kuna mbwa amemaliza kuku za wananchi kwenye kitongoji cha Mpanda kati kwa hiyo baada ya hapo tumeamua kuamka na kuanza kufukuzana na huyo mbwa, tulianza kufukuzana naye kuanzia saa kumi na mbili na kufika saa nne ya asubuhi wakati tunakaribia kumkamata akabadilika na kutokea binadamu" alieleza mwananchi

Afisa Mtendaji aliendelea kusimulia juu ya tukio hilo na kusema baada ya mbwa yule kubadilika na kuwa binadamu alianza kuongea akiwaomba wananchi wamuue na kukiri kuwa yeye ni mchawi na alitumwa.

"Baada ya hapo alijitambulisha anaitwa Happy Victor akaomba tusimrudishe kwao Ilemi bali tumuue na kusema kuwa mtoto wake anatuachia tumle sisi tukasema hapana hatuwezi kukuuwa ila tunakuomba utupe maelezo huku Mbozi umekujaje akasema huku nimekuja kuna mtu amenileta ila mama yangu ni mshirikina alichomewa nyumba kule Ilemi kwa hiyo mimi ni yule mbwa ambaye alipotea kule Ilemi aliyekuwa anatuhumiwa kwamba anakichaa. Sisi tukamsihi kwamba wewe basi sisi tunakuomba hizo nguo vaa akasema nikivaa hizi nguo nitabadilika kuwa mbwa yule wa kichaa" alisema Afisa Mtendaji

Kwa upande wake Afisa Tarafa ya Vwawa Haji Hamisi Ibrahamu amewataka wananchi kuachana na mambo ya kishirikina ambapo amewataka wazee wa mila na wachungaji wakemee tukio hilo na kusema kuwa mtu huyo wao watamfikisha kwenye vyombo vya sheria kwa kufanya uhalifu.

No comments:

Post a Comment