Chemical afunguka jinsi muziki wa singeli ulivyo mvunjia heshima.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 19 February 2018

Chemical afunguka jinsi muziki wa singeli ulivyo mvunjia heshima..

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Claudia Lubao ‘Chemical’, amefunguka kuwa kwa upande fulani Muziki wa Singeli, ulimpunguzia heshima kutoka kwa mashabiki wake ambao walikuwa wamekwisha muamini kupitia aina ya muziki wake alioanza nao wa kuchana.

Akizungumza Chemical alisema suala la kuimba Singeli lilitoka kwa menejimenti yake aliyoachana nayo, lakini kwa upande wake anaamini muziki wao unaweza kuwa umemuongezea mashabiki kidogo kwenye upande huo, lakini kwa mashabiki wake ambao tayari walikuwa wamekwisha mpokea vizuri kwenye Hip Hop, wamemshusha thamani.

“Ukweli ni kwamba siamini sana kupitia Muziki wa Singeli, ninaamini kwamba muziki wangu niliokuwa ninaufanya ulikuwa ni mkubwa kuliko Singeli,” alisema Chemical na kuongeza kuwa kwa sasa hafikirii tena kufanya muziki huo labda baadaye sana.

Mwaka jana, Chemical aliachia wimbo uitwao Kama Ipo Ipo Tu ambao kimsingi mwenyewe ameulalamikia kuwa umemshushia heshima. 

No comments:

Post a Comment