Young killer:Nilizinguliwa kisa Dogo Janja - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 11 January 2018

Young killer:Nilizinguliwa kisa Dogo Janja

RAPA anayefanya vizuri kwenye gemu la Hip Hop Bongo, Young Killer, amefunguka kuwa, katika harakati zake za muziki amewahi kukosa msaada wa kimuziki kisa akionekana anataka kuingia kwenye fani hiyo kumuiga Dogo Janja ambaye alikuwa ameshatoboa kimuziki.

Akizungumza Young Killer alisema kamwe hawezi kusahau alivyobaniwa na watu ambao wangeweza kumfanya atoke kimuziki muda mrefu, lakini alionekana anataka kuingia kwenye fani hiyo kwa kuwa ameona Dogo Janja anafanya vizuri kwenye gemu.

“Walidhani naingia kwenye muziki kwa sababu ya kumuiga Dogo Janja, nilibaniwa msaada nikionekana mkurupukaji, nilionekana kama nataka kufanya kwa kuwa nimeona mtoto mwenzangu anafanya, niliumia sana,”alisema Young Killer bila kuwataja watu hao. Killer alisema anashukuru Mungu alikuja kutoka kivingine na mashabiki wakamkubali.

No comments:

Post a Comment