Ouick Rocka amkana mpenzi wake hadharani - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday 11 January 2018

Ouick Rocka amkana mpenzi wake hadharani

Msanii Quick Rocka amekanusha tetesi zilizokuwa zikiendelea mitandaoni kuwa yupo kwenye uhusiano mzito wa kimapenzi na Muigizaji Alice Kella.

Rocka amekanusha tetesi hizo wakati amezungumza na kupinga kwamba tetesi ambazo zilianza kusambazwa na msanii Alice kwa kuweka picha mtandaoni na kuandika maneno "mume wangu nampenda sana" ambayo yalitafsiriwa kuwa ni wapenzi.

Aidha Quick Rocka amesema kwamba hakuna mahusiano yoyote ya kimapenzi kati yao bali picha ambazo zilisambaa ni sehemu ya kazi zao za filamu.

"Mimi na Alice hatuna mahusiano yoyote yale na zile picha ni series tu ambayo tunaifanya ndio tulikuwa tunafanya photoshoot na hakuna kingine chochote kinachoendelea kati yetu zaidi ya kazi na Alice ni kama mdogo wangu hivyo watu wasichukulie tofauti" Quick
Msanii Quick Rocka kwa sasa ni moja kati ya wasanii wakongwe na bado wanaendelea kufanya muziki na anafanya vizuri huku akiwa anasimamia kundi la muziki liitwalo OMG

No comments:

Post a Comment