Sanchi na mama yake wamekuwa gumzo mtandaoni - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 3 January 2018

Sanchi na mama yake wamekuwa gumzo mtandaoni

Modo maarufu Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’ na mama yake mzazi wamezua gumzo la aina yake mtandaoni baada kuanika picha zao mbalimbali. Gumzo hilo lilianza mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Sanchi kuweka picha mbalimbali akiwa na mama yake na watu wakaanza kuzijadili.

“Mh! Kwa kweli mama naye kaumbika, kumbe Sanchi kafuata kwa mama kila kitu, hebu angalia shepu, angalia mambo yetu ni hatarii,” aliandika mchangiaji mmoja mtandaoni. Kama hiyo haitoshi, wapo wengine waliomponda Sanchi kwa kitendo cha kumuweka mama yake mtandaoni ilhali anatambua fika siku zote yeye ni mtu wa picha chafu katika ukurasa wake wa Instagram. “Anamdhalilisha mama wa watu.

Yeye hakutakiwa kabisa kumposti mama yake maana watu wengi walikuwa wanajaribu kuhoji kwa binti mwenye wazazi iweje kila siku aposti picha za utupu?” alihoji mdau mtandaoni. Picha hizo zilisambazwa haraka sana mitandaoni ambapo wafausi wa mitandao mbalimbali waliibua mijadala mbalimbali huku wengine wakimsifu na kumponda. Kuhusu kuibua mjadala, Sanchi alipozungumza na mwanahabari wetu hivi karibuni, alisema hajali watu wanasema nini kuhusu yeye na mama yake na kwamba atakuwa akiposti picha kulingana na anavyojisikia.

No comments:

Post a Comment