Tanzania inatarajia kuwa wenyeji wa mkutano maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) utakaofanyika Februari 22 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Mkutano huo maalumu unaofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania unashirikisha nchi 19 wanachama wa Fifa.
Mkutano huo utakaoongozwa na Rais wa FIFA Gian Infantino pia utahudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Ahmad Ahmad, Makamu wa Rais wa Fifa, Katibu Mkuu wa Fifa na viongozi mbalimbali wa Fifa na CAF ikiwemo wajumbe wa kamati ya utendaji.
Wageni kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano huo wataanza kuwasili nchini Februari 20, 2018.
Ajenda za mkutano huo mkubwa wa Fifa ni miradi mbalimbali ya Fifa zamani ikifahamika kama Goal Project na sasa ikifahamika Fifa Forward Programme,ajenda ya soka la vijana, Wanawake na klabu wakati ajenda nyingine ya mkutano huo ni kujadili kalenda ya kimataifa ya Fifa,kuboresha masuala ya uhamisho na vipaumbele vyake
No comments:
Post a Comment