Yanga yapasua kichwa jinsi ya kuiangusha Simba SC - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 18 October 2017

Yanga yapasua kichwa jinsi ya kuiangusha Simba SC

Yanga imekumabana na wakati mgumu baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar wikiendi iliyopita ambapo wachezaji wake watano walipewa kadi za njano ambazo baadhi yao zimewaweka katika wakati mgumu kuweza kupishana na Simba.

Akili ambayo Yanga inataka kupiga sasa ni kuwaokoa mabeki wao wawili muhimu Kelvin Yondani na Juma Abdul ambao wote wapo katika kikosi cha cha kwanza wakiwa na kadi mbili za njano.

Mtego ambao Yanga italazimika kuukwepa ni endapo itajilipua na kuwapa nafasi katika mchezo ujao dhidi ya Stand, ambapo wawili hao wakipewa kadi yoyote itawafanya kuukosa rasmi mchezo unaofuata dhidi ya Simba Oktoba 28.

Akili ambayo imeanza kupigwa ni kutafuta mbadala wa mabeki hao ambapo huenda sura kama Hassan Ramadhan Kessy ataweza kuingia kuzb kwa Abdul huku mkongwe Nadir Haroub 'Cannavaro' na Abdallah Haji 'Ninja' wakifanyiwa mpango mmoja wao achukue nafasi ya Yondani.

Akizungumzia changamoto hiyo Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina tayari wameshaliona hilo ambapo watajua cha kufanya wakati utakapofika.

No comments:

Post a Comment