Shiza Kichuya aipeleka Simba SC kileleni - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday 5 November 2017

Shiza Kichuya aipeleka Simba SC kileleni

Mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya ameshusha presha ya mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuifunga Mbeya City bao 1-0 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo Jumapili.

Mwamuzi wa mchezo aliamuru mpira uwekwe kati baada ya shuti lililopigwa na Kichuya katika dakika ya saba ya kipindi cha kwanza kisha kuwainua mashabiki wa Simba waliokuwapo uwanjani hapo.

Simba imefikisha pointi 19 sawa na Azam FC ambayo ilishika usukani huo kwa muda baada ya jana jioni kuifunga Ruvu Shooting kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0.

Kikosi cha Joseph Omog kimefanikiwa kuendeleza kasi yake baada ya mchezo wao uliopita na watani zao Yanga kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

No comments:

Post a Comment