Okwi atemwa Uganda - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday 28 November 2017

Okwi atemwa Uganda

Mshambuliaji wa Simba na kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu Bara, Emmanuel Okwi ameachwa katika kikosi cha Uganda kitakachoshiriki mashindano ya Chalenji.

Wakati Okwi mwenye mabao nane katika kikosi cha Simba akiachwa Mganda mwenzake beki Juuko Murushid ndiye mchezaji pekee anayecheza nje ya Uganda aliyeitwa Cranes.

Kocha wa zamani wa Simba, anayefundisha Cranes, Moses Basena ameita wachezaji 26 kambini watakaopungua na kubaki 23 kabla ya safari ya Nairobi Jumamosi hii wakati mashindano yatafunguliwa Jumapili Desemba 3.

Mchezaji pekee anayecheza soka nje aliyeitwaa ni beki wa Simba, Murushid ambaye alikuwepo katika kikosi cha Uganda Cranes kilichoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) nchini Gabon.

Okwi hajaifungia Simba tangu Oktoba 15, alipofunga bao la kusawazisha dhidi ya Mtibwa Sugar na mwishoni mwa wiki hii alishindwa kuichezea timu ilipocheza dhidi ya Lipuli.
Kikosi cha Uganda:

Makipa: Isma Watenga (Vipers SC), Benjamin Ochan (KCCA), Nichoals Sebwato (Onduparaka FC) Ikara Tom (Kirinya Jinja)
Mabeki: Nico Wakiro Wadada (Vipers), Ibrahim Kiyemba (Sc Villa Jogoo), Isaac Muleme (KCCA FC), Aggrey Madoi (Police), Juuko Murushid (Simba-Tanzania), Timothy Awanyi (KCCA FC), Savio Kabugo (Proline FC), Bernard Muwanga (Sc Villa Jogoo)
Viungo: Tom Masiko (Vipers), Mutyaba Muzamiru (KCCA), Tadeo Lwanga (Vipers), Karisa Milton (Vipers), Paul Mucureezi (KCCA), Albert Mugisa (Police), Allan Kateregga (KCCA FC), Allan Kyambadde (Sc Villa Jogoo),Saddam Juma (KCCA )
Washambuliaji: Nelson Senkatuka (Bright Stars), Derick Nsibambi (KCCA), Hood Kaweesa (Police), Seif Batte (Bright Stars), Daniel Isiagi Opolot (Proline), Methodious Bassey (Mbarara City).

No comments:

Post a Comment