Mchumba wa Ndikumana amduwaza Uwoya - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday 22 November 2017

Mchumba wa Ndikumana amduwaza Uwoya

Hamad Ndikumana ‘Ndiku’ enzi za uhai wake.
Mchumba wa marehemu Hamad Ndikumana ‘Ndiku’, Asma amemduwaza mzazi mwenzake na marehemu huyo, muigizaji Irene Uwoya baada ya kumpa mapokezi ya nguvu msanii huyo aliyewasili nchini Rwanda hivi karibuni kuhani msiba.

Kwa mujibu wa chanzo makini, mchumba huyo wa Ndiku alimduwaza Uwoya kwani mbali na kumpokea vizuri alikuwa rafiki ghafla na kuzungumza naye kirafiki, kumuonesha mazingira yote ya kule tofauti na jinsi Uwoya alivyotarajia kwa tabia za wanawake wengine. “Yani Uwoya hakutegemea kabisa kama Asma anaweza kumpokea vile.
Irene Uwoya.
Hakuonesha kinyongo chochote cha kike kama ambavyo wengi wanajua wanawake wanapokutana, hususana kama hawa ambao inafahamika wameshea mwanaume. “Alikuwa mchangamfu kupita maelezo, alimuonesha mitaa na kila walipokuwa wanakwenda walikuwa pamoja utafikiri wamejuana muda mrefu kumbe wala, ghafla wakajikuta wamelikubali tatizo lililotokea na kuona hakuna sababu ya kununiana kwanza ukizingatia wameshajua chanzo cha kifo cha Ndiku ni wanasoka wenzake,” kilisema chanzo hicho.

Taarifa zinaeleza kuwa, familia ipo katika hatua za kisheria kuwashughulikia wote wanaotajwa kuhusika na kifo cha Ndiku kinachosadikika kimetokana na kulishwa sumu Akizingumza  Uwoya alisema anamshukuru Mungu kupokelewa na Asma jambo ambalo kidogo lilimfanya aduwae kwani hakutarajia kukutana na mwanamke ambaye alikuwa mchumba wa Ndiku na kumjali kiasi hicho.

Ndikumana alikutwa na umauti Novemba 14, mwaka huu usiku saa chache baada ya kutoka kwenye mazoezi ya timu yake ya Rayon Sports, timu ambayo alikuwa akiitumikia kama kocha msaidizi. Taarifa za awali za kidaktari zilieleza kuwa, Ndikumana ambaye alifunga ndoa na Uwoya mwaka 2009, alifariki kutokana na kuwa na tatizo la moyo.

Marehemu Ndikuma na Uwoya walioishi kwa miaka kadhaa ya ndoa kisha kutengana, walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume (Krish) ambaye anasoma hapa nchini, wakati marehemu baba yake alikita maskani yake nchini mwao, Rwanda

No comments:

Post a Comment