Chuchu atoa povu hili zito kuhusu kuachana na Ray - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 17 November 2017

Chuchu atoa povu hili zito kuhusu kuachana na Ray

STAA wa filamu Bongo, Chuchu Hans kwa mara ya kwanza amegeuka mbogo ‘amewaka’ baada ya kuulizwa madai ya kuachana na msanii mwenzake aliyezaa naye mtoto mmoja, Vincent Kigosi ‘Ray’.

Chuchu amesema kuwa, kila kukicha anasikia madai ya kuachana na mzazi mwenzie huyo na mpaka sasa hajajua ni nani anayeendelea kuzusha habari hizo.

“Najua wazi watu wengi hawapendi kabisa kuniona na Ray. Naanza kuingiwa na wasiwasi huenda wanaosambaza habari hizo ni watu wa karibu yetu na siku nikiwabaini ama zake au zangu,” aliwaka Chuchu.

No comments:

Post a Comment