CAF imesogeza mbele Uganda na Taifa Stars - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 23 November 2017

CAF imesogeza mbele Uganda na Taifa Stars

Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limesogeza mbele hadi Machi 2019, michezo ya raundi ya pili kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) ikiwemo mechi kati ya Uganda na Tanzania 'Taifa Stars'
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Caf, uamuzi wa kusogeza mbele kwa mwaka mzima michezo ya raundi hiyo ni kuzipa nafasi timu tano za Afrika zilizopata nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Russia kuanzia Juni mwakani.

Kutoka na kusogezwa mbele kwa mechi za raundi hiyo, mchezo utakaofuata wa Stars katika harakati za kuwania kufuzu mashindano ya Afcon 2019 ambayo yatafanyika Cameroon, utakuwa wa ugenini dhidi ya Cape Verde ambao utafanyika katika ya Juni 5 hadi 13, 2017.

Kati ya Septemba 3-11, 2018 Stars itakuwa nyumbani kuwakaribisha Cape Verde na mchezo utakaofuata utakuwa dhidi ya Lesotho ugenini ambao utachezwa kati ya Oktoba 8-16, 2018 na baada ya hapo itacheza nyumbani dhidi ya Uganda ambao utafanyika kati ya Novemba 12 hadi 20, 2018.

No comments:

Post a Comment