Yanga yaiponza Simba mechi ya Jumapili - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 11 October 2017

Yanga yaiponza Simba mechi ya Jumapili

KITENDO cha Yanga kukubali kulazimishwa suluhu Mtibwa Sugar, kimewaponza watani zao Simba ambao wikiendi hii watakutana na mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu.

Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema sare dhidi ya Yanga imewapa hali ya kujiamini kuwa wanaweza kufanya vizuri pia dhidi ya Simba na kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo katika mechi 13 mpaka sasa.

"Msimu huu tunataka uwe wa tofauti na iliyopita ndiyo maana tunataka kuanza na wababe kisha tutarejea kupambana na wa huku chini, hilo linawezekana kikubwa ni dhamira ya dhati," alisema.

No comments:

Post a Comment