Vanessa Mdee ameshindwa kuvumilia kisa Jux, ametoa povu kali - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 11 October 2017

Vanessa Mdee ameshindwa kuvumilia kisa Jux, ametoa povu kali

 Msanii Vanessa Mdee ameshindwa kuvumilia maneno ya shabiki mmoja kwenye account ya Instagram ya Jux na kuamua kumtolea povu juu ya maneno yake ya shombo kwa mpenzi wake wa zamani huyo.

Jux aliweka video akifanya show ya pamoja na Vanessa Mdee na moja ya shabiki wa Jux wa kike alianza kumponda Jux kuwa anajipendekeza kwa Vanessa na kwenda mbali zaidi na kusema Vanessa hana haja na yeye na hana kitu cha kumpa.

Kufuatia ujumbe huo Vanessa Mdee alishindwa kuvumilia na kuja kumjibu binti huyo kwa kumweleza kuwa yeye si msemaji wake na kudai amekuwa akitukana kila siku kwenye page hiyo ya Jux na kusema huenda akawa anamtaka Jux.



Juma Jux na Vanessa Mdee walikuwa ni wapenzi lakini baadaye ikasemakana kila mmoja kuanza maisha yake mapya, ingawa wapo watu wanadai kuwa wawili hao ni wapenzi ila wameamua kuweka maisha yao ya mapenzi chini ya kapeti ili kutoa nafasi zaidi ya kazi zao za sanaa kupata nafasi zaidi kuliko kuzungumziwa zaidi kwenye mapenzi na mahusiano.

No comments:

Post a Comment