Yanga kuonyesha maujuzi yao kwa Kagera Sugar - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 11 October 2017

Yanga kuonyesha maujuzi yao kwa Kagera Sugar

STRAIKA wa Yanga, Emmanuel Martin ameelezea jinsi ilivyo ngumu kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, akieleza sababu inatokana na kila mchezaji kutaka kuonyesha ufundi wake.

"Si kazi nyepesi mchezaji kufanikiwa kucheza ndani ya kikosi cha kwanza, kwani kina ushindani wa hali ya juu, hilo limenifunza kuwa na nidhamu ninapoaminiwa kucheza bila hivyo inakuwa ni kusubiri wenzako wafanye kazi,"anasema.

Anasimulia ushindani anaouona tangu ajiunge na Yanga akitokea JKU ya Zanzibar, kwamba umekuwa ukiongezeka siku hadi siku, jambo analoamini litamsaidia kutimiza ndoto zake za kufika mbali zaidi ya alipo.

"Unapokumbana na ugumu unatia akili kuthamini kazi na kujua hakuna kitu ambacho ni lele mama ndiyo maana naona unanisaidia kila wakati kujituma na kutojisahau," anasema.

Kuhusiana na mechi iliyopo mbele yao na Kagera Sugar, wakicheza ugenini amesema watapambana inavyowezekana wakijua wapinzani wao wana hamu ya kushinda mchezo huo.

"Ikumbukwe Kagera Sugar, hawakuwa na matokeo mazuri tangu wameanza ligi ya msimu huu, hilo litapelekea kila mchezaji kujituma kadri awezavyo ili kupata matokeo," anasema.

No comments:

Post a Comment