Juma Liuzio amekiri Simba kuwa na ushindani mkali - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 11 October 2017

Juma Liuzio amekiri Simba kuwa na ushindani mkali

Mshambuliaji wa Simba, Juma Liuzio amekiri kuwa kikosi chao kina ushindani mkubwa kwa msimu huu tofauti na msimu uliopita.

Liuzio ambaye ameifungia Simba bao moja katika mechi tano za msimu huu, alisema eneo la ushambuliaji lina changamoto kubwa lakini bado nafasi yake kucheza ni kubwa.

"Kocha anafanya mabadiliko kadhaa kila wakati, kurejea kwa Laudit Mavugo pia kunaongeza ushindani," alisema.
"Hata hivyo sina mashaka na nafasi yangu, nafahamu kuwa nitacheza tu, tena mechi nyingi," alisema.

No comments:

Post a Comment