Watu 20 wauawa 100 wajeruhiwa Las Vegas Marekani kwa kupigwa risasi. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 2 October 2017

Watu 20 wauawa 100 wajeruhiwa Las Vegas Marekani kwa kupigwa risasi.

WATU zaidi ya 20 wameuawa na 100 kujeruhiwa wakati mtu mwenye bunduki alipofyatua mamia ya risasi kutoka ghorofa ya 32 ya hoteli ya Mandalala Bay kwenye tamasha la muziki huko Las Vegas, Marekani.

Mtu huyo aliuawa na polisi mara moja ambapo ‘mwenzake’, mwanamke mwenye asili ya Asia anatafutwa.

Miongoni mwa watu waliokufa ni pamoja na polisi wawili waliokuwepo kwenye tamasha hilo ambalo lilihudhuriwa na watu 30,000.

Eneo hilo limefungwa baada ya mauaji hayo kwenye tamasha hilo lijulikanalo Route 91 Harvest ambapo polisi wanaamini kwamba risasi hizo zilipigwa na mtu mmoja.

Polisi walisema walimuua mtu aliyefyatua risasi hizo na wanamtafuta mwanamke aitwaye Marilou Danley ambaye wanaamini atausaidia uchunguzi wao tukio hilo.

Msemaji wa polisi alizima uvumi kwamba kulikuwa na mashambulio mengine na ulipuaji wa mabomu, akasema pia muuaji huyo ametambuliwa kuwa ni mkazi wa eneo hilo.

No comments:

Post a Comment