Simba inasubiria point tatu muhimu kutoka FIFA - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 13 October 2017

Simba inasubiria point tatu muhimu kutoka FIFA

Dodoma Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara ikiendelea wikiendi hii kwa mechi za raundi ya 6 na msimamo wa ligi ukionyesha timu ya Simba inaongoza, lakini taarifa kutoka kwenye uongozi wa timu hiyo ni kwamba bado wanaendelea kusubiria majibu ya barua yao waliyoiandikia Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Kupitia Idara ya Habari na Mawasiliano ya timu hiyo ya Simba inayoongozwa na Haji Manara ni kwamba barua yao waliyoipeleka Fifa yenye shauri lao la kupokwa pointi 3 walizozichukua awali dhidi ya timu ya Kagera Sugar bado hawajajibiwa na wanaamini kuna siku shirikisho hilo litawajibu.

“Ni kweli Simba tulipeleka malalamiko Fifa ila hayajaja,tulipeleka barua maalum kwao bado majibu hayajarudi na tulipeleka kwa msingi kwamba kamati ya hadhi na sheria iliyotupoka pointi zetu 3 haikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri la ndani ya uwanja hivyo tunasubiria bado,” alisema Manara.

Katika hatua nyingine Manara alisema kuwa licha ya kwamba bado wanasubiri uamuzi wa Fifa juu ya shauri lao hilo wao hawana shaka yoyote bali wanachowaza zaidi kwa sasa ni timu hiyo kufanya vizuri kwenye mechi zao za ligi ili wachukue ubingwa msimu huu.

“Fifa bado haijatujibu hivyo tunasubiri wakitujibu tutasema wakiturudishia pointi zetu itakuwa sawa na wasipoturudishia sawa tu kwanza hata tukikabidhiwa ubingwa wakati huu hauna raha kwakua lengo letu sasa ni kuendelea kushinda mechi zetu za ligi inayoendelea,” alisisitiza Manara.

Simba keshokutwa Jumapili itakuwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam itakapotifuana na wapinzani wao Mtibwa Sugar ambao wanalingana pointi 11.

No comments:

Post a Comment