Tokea mwaka 2012 siku ambayo Simba iliishinda Yanga kwa mabao 5-0, hadi leo kiungo Haruna Niyonzima ameendelea kuweka kumbukumbu ya jezi ya Simba iliyochezewa siku hiyo.
Jezi ya Simba aliyoihifadhi ni ya kiungo Mutesa Mafisango aliyefariki kwa ajali ya gari siku chache baadaye.
Niyonzima ambaye amejiunga na Yanga akitokea Simba, amesema ameiweka jezi hiyo hadi leo.
“Hadi leo nimeihifadhi kwa heshima kubwa. Mafisango alikuwa ni kama kaka yangu kabisa,” alisema.
“Baada ya mechi siku hiyo alikuja moja kwa moja na kunipa jezi yake akisema ni zawadi kwangu.
“Nilicheza na Mafisango APR na timu ya taifa ya Rwanda, yeye akiwa nahodha na mimi msaidizi.”
Niyonzima ni mtu anayependa kuweka kumbukumbu hasa katika vitu mbalimbali anavyovipata katika mpira.
No comments:
Post a Comment