Mc pilipili baada ya harusi ya joti' Nilitamani nioe ila sijapata Mchumba' - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday 31 October 2017

Mc pilipili baada ya harusi ya joti' Nilitamani nioe ila sijapata Mchumba'

Mchekeshaji Mc Pilipili ameweka wazi mipango yake ya ndoa kwa kueleza mwakani atafunga ndoa.

Kauli ya Mc Pilipili inakuja mara baada ya mchekeshaji mwenzie, Joti kufunga ndoa mwishoni mwa weekend iliyopita, October 28, 2017.

“Nilipenda nioe mwaka huu mwezi wa 10 na kwa sababu mwezi umefika bado sijapata mchumba, lakini mwezi wa 10 mwakani kitu kikubwa kitatokea” amesema Mc Pilipili.

Katika hatua nyingine Mc Pilipili amesema si vizuri kwa kina dada kuwachukulia wachekeshaji kama watu wasio serious katika mahusiano kwani hata wao wana nyoyo za kupenda pia.

No comments:

Post a Comment