Maggie Vampire afunguka jinsi alivyopata shavu la kuonekana kwenye video mpya ya Davido - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday 31 October 2017

Maggie Vampire afunguka jinsi alivyopata shavu la kuonekana kwenye video mpya ya Davido

Mrembo wa kupamba video Bongo, Maggie Vampire amefunguka alivyopata dili la kuonekana katika video mpya ya msanii wa Nigeria, Davido.

Akiongea na gazeti la Bingwa, Maggie amesema wakati anapata dili hilo hakuwa anafahamu kama video hiyo itakuwa ya Davido mpaka pale alipofika location kisiwani Zanzibar ndio akafahamu hilo.

“Nilitafutwa nikaambiwa kuna video Zanzibar inatakiwa nikafanye, nikaambiwa nitalipwa bei fulani na mimi nikaridhika nikaenda. Sikujua kama ni Davido, ile nafika tu nakutana na Davido ilikuwa ni surprise kwangu,” amesema mrembo huyo.

“Kiukweli Davido ni mtu poa sana na suala la malipo na malazi yalikuwa mazuri tofauti na wasanii wetu wa Bongo na tulifanya video ile kwa siku mbili,” ameongeza.

No comments:

Post a Comment