Lwandamina kaamua hatima ya mkongo - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 9 October 2017

Lwandamina kaamua hatima ya mkongo

Dar es Salaam. Kama kocha wa Yanga, George Lwandamina atatoa taarifa rasmi kwa uongozi juu ya hatma ya beki Mkongomani, Fiston Kayembe, uongozi wa klabu hiyo utampatia mkataba wa kuitumikia timu hiyo mara moja.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema wanasubiri ripoti ya kocha huyo ili waweze kumalizana na beki huyo ambaye ataziba nafasi iliyoachwa wazi na beki Mtogo, Vincent Bossou.

"Tulikuwa tunasubiri kocha amuone katika mechi za kirafiki. Tunashukuru kwamba amecheza dhidi ya KMC na kama kocha atasema anafaa tutamsajili," alisema Mkwasa.

"Kwa utaratibu tulionao mchezaji ni lazima apitishwe kwanza na kocha, hatuwezi kumsaini mtu bila kupata kibali. Tutamalizana naye mapema tu kama tukipata ruhusa hiyo," alifafanua.

No comments:

Post a Comment