Donald Ngoma Njee kwa muda wa takribani wiki moja. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 3 October 2017

Donald Ngoma Njee kwa muda wa takribani wiki moja.

MSHAMBULIAJI Mzimbabwe wa Yanga, Donald Dombo Ngoma atahitaji mapumziko ya wiki moja tu kabla ya kuanza tena mazoezi kufuatia kuumia Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

Ngoma aliondoka uwanjani anachechemea dakika ya 77 Jumamosi Yanga ikilazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Mahadhi.

Na baada ya hapo, mchezaji huyo akaenda kufanyiwa vipimo jana na kugundulika amepata misuli ya ndani ya paja ilivutika siku hiyo na kumsababishia maumivu kwa mujibu wa Daktari wa Yanga, Edward Bavu.

“Misuli ya ndani ya paja ilivutika na kumsababishia maumivu, lakini tayari ameanza matibabu na tunatarajia atarejea kuanza mazoezi baada ya wiki moja tu, si maumivu makubwa kama ilivyofikiriwa,”alisema Dk. Bavu.

Daktari huyo wa Yanga amesema kwamba hayo ni maumivu mapya kabisa kwa Ngoma tofauti na yale yaliyomuweka nje kwa muda mrefu msimu uliopita ya goti.
Ligi Kuu imesimama kwa sasa kupisha mechi za kimataifa za kufuzu Kombe la Dunia na za kirafiki kwa nchi ambazo zimekwishatolewa kwenye mbio za Urusi 2018, ikiwemo Tanzania.

Na Jumamosi wiki hii, Taifa Stars itakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Yanga itateremka tena uwanjani Oktoba 14, kumenyana na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

No comments:

Post a Comment