Amber lulu: Prezoo hakupata hata chembe ya Penzi kutoka kwangu. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 9 October 2017

Amber lulu: Prezoo hakupata hata chembe ya Penzi kutoka kwangu.

Video Vixen na msanii wa muziki wa Bongo Flava, Amber Lulu amesema si kweli alitoka kimapenzi na rapper Prezoo kutoka nchini Kenya ambaye alikuwa hapa nchini siku za hivi karibuni.

Wiki iliyopitia katika mitandao kulisambaa clip ya video ikionyesha wawili hao wakiwa katika mahaba mazito ndani ya gari na video nyingine wakiwa chumbani.

Akizungumza na FNL ya EATV Amber Lulu amesema hakuna lolote liloendelea kati yao kwani Prezoo ni rafiki wa kawaida.
“Watu wengine washamba lakini ni vitu fulani vya kinyamwezi tu ambapo unaweza ukakaa na mtu chumba kimoja na msifanye kitu chochote,” amesema Amber Lulu.

Aliongeza kuwa ndege wawili wanaofanana huwa wanaruka pamoja kwa hiyo Prezoo ni kama rafiki kwake na hakuna tatizo la wao kuwa hivyo.

Aliendelea kwa kusema nyumba walikuwa pamoja ni kama apartment ambapo kila mmoja alikuwa na chumba chake.

No comments:

Post a Comment