Ajibu jiongeze kuwashangaza watanzania - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 14 October 2017

Ajibu jiongeze kuwashangaza watanzania

MTANZANIA anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Tusker FC ya Kenya, Abdul Hassan, amemshika sikio nyota wa Yanga, Ibrahim Ajibu kuwa ana kila kitu kiufundi hivyo aanze kufikiria kucheza nje.

Hassan alijiunga na Tusker ya Kenya Januari mwaka huu akitokea African Lyon, alijumuishwa kwenye kikosi cha Stars kilichocheza na Malawi hivi karibuni na kubaini kwa ukaribu ufundi wa Ajibu.

“Wachezaji wa Tanzania ni waoga wa kuthubutu kutoka nje, ila tuna vipaji vya aina yake ambavyo vinaweza kuwa gumzo kimataifa, mtu kama Ajibu anaweza akashangaza wengi na Tanzania ikaendelea kuheshimika kupitia yeye kama ilivyo kwa Mbwana Samatta huko Ubeligiji ,”alisema.

Alijitolea mfano yeye mwenyewe kwamba aliamua kuthubutu licha ya Lyon aliyokuwa anaichezea kushuka daraja, lakini hakuamini kama kiwango chake kimeshuka na timu.

“Nikaamua kuangalia soka la nje, lililonisaidia kupata nafasi ndani ya kikosi cha Stars, nawashauri na wengine wajaribu kutoka waachane na uoga soka kwa sasa ni biashara nzuri ya kumfanya mchezaji atembee masafa marefu kutokana na sayansi na tekinolojia kukua,” alisema.

No comments:

Post a Comment