Klabu ya Yanga imeeleza kuwa imejiandaa vyema kuelekea mchezo wa ligi kuu ya soka Tanznaia Bara kesho dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Akiongea na Wanahabari leo kwenye makao makuu ya klabu msemaji wa Yanga, Dismass Ten amesema timu hiyo imejiandaa vya kutosha na inahitaji pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo.
“Timu imejiandaa vizuri, sisi ni mabingwa watetezi kwahiyo tunahakikisha tunachukua pointi tatu muhimu na hatutadharau mechi”, amesema Ten.
Aidha kocha msaidizi wa timu hiyo Shadrack Nsajigwa amesema wachezaji wote wapo vizuri isipokuwa Amis Tambwe ambaye alikuwa majeruhi lakini tayari ameshapata kibali cha daktari na anaendelea vizuri na mazoezi.
Yanga ambayo ipo nafasi ya sita ikiwa na alama 8 itamkosa nyota wake wa Kimataifa kiungo Tshishimbi Kabamba ambaye anatumikia adhabu ya kukosa mechi moja baada ya kupata kadi 3 za njano katika mechi 3 zilizopita.
No comments:
Post a Comment