Ujue umri wa mwisho kushiriki Tendo la Ndoa. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday 30 September 2017

Ujue umri wa mwisho kushiriki Tendo la Ndoa.

WENGI huwa wanajiuliza mwanamke au mwanaume, umri wa mwisho kushiriki tendo la ndoa ni upi? Ukiwa mzee unaweza kushiriki tendo hili hadi lini? Kuna madhara yoyote kwa bibi au babu kikongwe kuendelea kushiriki? Katika kujibu maswali haya ni vema kupitia baadhi ya tafiti ambazo zilifanyika duniani ili kupata ukweli wa maswali.

HALI HALISI ILIVYO
Kila binadamu ambaye ameshazoea kuwa karibu na mwenza wake siku zote
angependa iwe hivyo. Hii ni pamoja na kuendelea kuwa na hamu ya tendo la ndoa, uwezo wa kufanya tendo la ndoa na kuridhishwa na tendo la ndoa, lakini kadiri umri unavyoongezeka yanatokea mabadiliko ambayo yanaweza kuleta matatizo usiyotarajia.

MABADILILIKO YA KAWAIDA UZEENI
Mabadiliko ya kawaida uzeeni humbadilisha mwanaume na mwanamke muonekano wao katika maumbile kuanzia nje hadi sehemu za siri. Mabadiliko haya ya kawaida pia hupunguza mvuto wa kuwa na hamu ya tendo la ndoa. Mwanamke anapozeeka huhisi mabadiliko yasiyo ya kawaida ukeni ambapo uke huanza kuwa na kina kifupi na upana wa mwingilio hupungua, ngozi ya ukeni huwa nyembamba sana tofauti na awali na huwa ngumu, haitanuki kama mwanzo. Majimaji ya ukeni yanayolainisha uke huanza kupungua taratibu. Hali hii huondoa uwezo wa kufanya tendo la ndoa na hali ya kulifurahia.

Kwa hiyo ukiona hali hii inaanza kukutokea basi wasiliana na daktari wako. Kwa upande wa wanaume wanapoanza kuzeeka nguvu za kiume huanza kupungua na kupotea, hali hii ndio kiashiria kikubwa cha kuzeeka kwa mwanaume. Upungufu wa nguvu za kismet ambao kitaalamu tunaita Erectile Dysfunction humfanya mwanaume uume wake usiwe na nguvu za kutosha kuhimili ufanyaji wa tendo la ndoa kwa muda mrefu.

Unaposimama uume hauwi imara na mkubwa kama inavyotakiwa na huwa unapwaya, ingawa tatizo hili siyo tu hutokea uzeeni.
UMRI WA UZEE
Labda tujiulize, umri wa uzee ni upi ambao tunasema mtu anashindwa au anaanza kushindwa kufanya tendo la ndoa? Kwa mujibu wa utafiti, umri wa uzee ambao tunategemea mwanaume na mwanamke wanaweza kupata matatizo haya ni kuanzia miaka sitini endapo watu hawa walikuwa na afya nzuri tangu ujana wao. Unaweza kupata mabadiliko na matatizo katika tendo la ndoa hata katika umri wa ujana au kabla ya umri wa miaka sitini endapo utakuwa na matatizo mbalimbali ya kiafya. Utafiti mwingine unaonyesha kuwa idadi kubwa ya matatizo haya hutokea katika umri wa miaka 35 hadi 55, hii ni kwa wote wanaume na wanawake kutokana na sababu mbalimbali.

MAGONJWA YA WAZEE YANAYOATHIRI UFANYAJI WA TENDO LA NDOA
Wazee kuanzia umri wa miaka sitini husumbuliwa na magonjwa mbalimbali kama tutakavyoona. Matumizi ya baadhi ya madawa kwa muda mrefu kutokana na matatizo mbalimbali pia huwaathiri na endapo walishawahi kufanyiwa upasuaji katika viungo vyao vya uzazi.

Matatizo ya kimahusiano na mpenzi wako pia huweza kukuathiri. Kwa hiyo matatizo haya tunategemea tunayapata kwa wazee endapo utajikuta unapata matatizo haya na wewe upo katika umri wa chini ya miaka sitini basi ujue mwili wako unaanza kuchoka na unatakiwa ufanyiwe uchunguzi wa kina. Magonjwa ya wazee yanayoathiri uwezo wa kufanya tendo la ndo ni kama vile: Arthritis: Ni maumivu ya mifupa mwilini katika sehemu za maungio, hasa magoti, viwiko vya mikono, mabega, kiuno na mgongo. Ni vema wazee wawe na tabia ya kufanya mazoezi kidogokidogo, kupumzika na kila wakati wanapooga waoge maji ya uvuguvugu. Ni vizuri wapate tiba kwa matatizo hayo.

No comments:

Post a Comment