Shilole adaiwa kumtesa Uchebe. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 29 September 2017

Shilole adaiwa kumtesa Uchebe.


MKALI wa miondoko ya Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ anadaiwa kumtesa mpenzi wake, Ashiraf Uchebe na kwamba imefikia kipindi anamgombeza mbele za watu kama mtoto mdogo. Kwa mujibu wa chanzo, kiliitonya Star Mix kuwa, juzikati katika Ukumbi wa Maisha Basement, Kijitonyama jijini Dar, Shilole alionekana akimkoromea Uchebe.

“Yaani hadi aibu, Shilole sijui kwa nini aliamua kufanya vile, kuna wakati alikuwa akimnyooshea vidole na kumsuka,” kilisema chanzo kilichohudhuria ukumbini hapo.

Star Mix baada ya kuunyaka ubuyu huo, ilimvutia waya Shilole ambapo alisema; “Jamani watu wanajua kukuza mambo na kuniona kama mimi ni mkorofi kila wakati kwenye mapenzi, lakini siamini kabisa kwenye mapenzi hakuna ugomvi wala purukushani kwani vyote nisehemu ya mapenzi.”

No comments:

Post a Comment