OMBI LA HAJI MANARA WA SIMBA SC KWA RC MAKONDA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 4 September 2017

OMBI LA HAJI MANARA WA SIMBA SC KWA RC MAKONDA.

Haji manara amemuomba mkuu wa mkoa wa Dar es salaam RC Makonda kusimamia na kupinga uuzwaji wa jezi feki.

Amesema kwenye vyombo vya habari kuwa“kwa muda wa miaka miwili klabu ya simba pasipo na shaka lolote tumekuwa klabu pekee Tanzania ambayo ukiiona tu jezi ile unajua ni ya simba,sizungumzii colour za kijani na njano wanajua yanga.

Lakini kwa sasa kumekuwa na jezi feki, nimuombe mkuu wa mkoa asimamie kwani simba ipo hapahapa Dar es salaam kwahiyo kupitia vyombo vya habari simba imuombe kukamata watu wanaofyatua jezi feki kwani kwa sasa pesa hatupati kupitia getini bali ni uuzaji wa jezi,suala zima tunaiachia mamlaka husika”

maneno ya Haji Manara wa simba kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

No comments:

Post a Comment