Kiungo wa Simba, Niyonzima, sasa yuko fiti na anachosubiri ni uamuzi wa Kocha Joseph Omog kama acheze mechi dhidi ya Mbao FC .
Niyonzima ambaye alikuwa majeruhi, alikuwa amefanya mazoezi siku mbili kabla ya Simba kuivaa Mwadui FC na kushinda kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Leo, Niyonzima amejifua na wenzake kwenye Uwanja wa Alliance katika kitongoji cha Mahina jijini Dar es Salaam.
Simba iko jijini humo kwa ajili ya mechi yake dhidi ya Mbao FC itakayopigwa keshokutwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
No comments:
Post a Comment