MECHI YA SIMBA NA AZAM IMERUDISHWA NYUMA MUDA SAA 10;00 JIONI KWA SABABU ZA KIUSALAMA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 8 September 2017

MECHI YA SIMBA NA AZAM IMERUDISHWA NYUMA MUDA SAA 10;00 JIONI KWA SABABU ZA KIUSALAMA.

MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji Azam FC na Simba SC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, umerudishwa Saa 10:00 jioni kutoka Saa 1:00 usiku.

Hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu za kiusalama, baada ya Jeshi la Polisi Tanzania kusema kwamba ni hatari mechi hiyo kuchezwa usiku na imeliagiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuirudisha Saa 10:00 jioni.

Mambo mengine yote yanabaki kama yalivyopangwa na mchezo huo utachezeshwa na refa Ludovick Charles wa Tabora, atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Abdallah Mkomwa wa Pwani na mezani atakuwepo Josephat Bulali na Kamisaa atakuwa Ruvu Kiwanga, wote wa Dar es Salaam, wakati viingilio ni Sh. 10,000 kwa jukwaa la VIP na 7,000 kwa mzunguko.

Timu zote zilianza kwa ushindi katika mechi zao za kwanza Ligi Kuu, Azam FC wakishinda 1-0 ugenini dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara huku Simba wakishinda 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Na kesho makocha wa timu zote, Mcameroon Joseph Marius Omog na Mromania Aristica Cioaba watataka kuendeleza wimbi la ushindi katika jitihada za kuipokonya taji Yanga SC.

No comments:

Post a Comment