Haji Manara:Omog kaivuruga yanga. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 28 September 2017

Haji Manara:Omog kaivuruga yanga.

Haji Manara amefunguka na kusema Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog anahitajika zaidi na Simba kuliko hata yeye anavyohitaji Simba na kudai ni kocha pekee aliyeweza kuipa Simba vikombe viwili na kuifunga Yanga mara tatu katika mechi nne walizokutana.

Manara amesema hayo jana wakati akielezea mambo mbalimbali kuelekea mchezo wao na Stand United ambao unatarajiwa kupigwa katika uwanja wa Kambarage Shinyanga ambapo amedai wanaiheshimu timu hiyo lakini wao wanakwenda kwa lengo la kutafuta pointi tatu.

"Makocha watano wamekaa hapa Simba wameshindwa kutupa nafasi ya pili, wameshindwa kutupa kikombe lakini Omog katupa vikombe viwili na vyote kamnyang'anya Yanga kakutana na Yanga mara nne kampiga mara tatu, halafu kuna mtu mtaani anasema Omog hafai, Simba sasa hivi inamuhitaji zaidi Omoh kuliko Omog anavyoihitaji Simba kwa sasa" alisema Haji Manara

No comments:

Post a Comment