Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo anafanya maombi ya kumuombea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ikiwa bado hali yake bado haijatengemaa, yameibuka maswali kadhaa kuhusu shambulio dhidi yake lililotokea Alhamisi iliyopita mjini Dodoma.
Watu wasiojulikana walimshambulia rais huyo wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kwa risasi zipatazo 32 akiwa ndani ya gari lake baada ya kuwasili katika makazi yake eneo la Area D, na ni risasi tano zilizompata na kumjeruhi vibaya.
No comments:
Post a Comment