"WET" YAMPA KICHEKO VEE MONEY. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 1 May 2018

"WET" YAMPA KICHEKO VEE MONEY.

Vanessa Mdee ‘Vee Money’,
MWANADADA ambaye kwa sasa anafanya vyema na album iitwayo Money Mondays, Vanessa Mdee ‘Vee Money’, hivi karibuni amechekelea views katika mtandao wa YouTube ambazo wimbo wake namba 9, kwenye album yake uitwao Wet, umepata.
Wimbo huo ambao video yake ilifanywa na prodyuza kutoka Afrika Kusini, Justin Compas, ukiwa na wiki mbili tu umeweza kutazamwa na watu zaidi ya milioni moja jambo ambalo lilimfanya Vee Money kuandika hivi kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram;
“1 Million views in 2 weeks. #Wet. Kwangu mimi ni kitu kikubwa tena sana. (Nimesema kwangu mimi).”
Mbali na maandishi hayo Vee Money aliwashukuru pia mashabiki wake ambao wanampa sapoti katika kazi zake za muziki kila kukicha.

No comments:

Post a Comment