SERIKALI YATOA FURSA HII KWA WANAHABARI. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 3 May 2018

SERIKALI YATOA FURSA HII KWA WANAHABARI.

Waziri wa Habari, Utamaduni na michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema Serikali imefungua milango ya majadiliano na wanahabari kuhusu changamoto zao. 
Waziri Mwakyembe amesema hayo leo katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ambapo ameweka wazi kwamba Serikali imetoa haki ya kupelekwa mahakamani mashauri mbalimbali kuhusiana na sheria ambazo zimepitishwa lakini bado kuna fursa nzuri ya kufanya mazungumzo na wadau.
Serikali itaendelea kusimamia sheria zilizotungwa katika kuhakikisha wanahabari na wamiliki wa mitandao ya kijamii wanafanyakazi kwa weledi na kujali maslahi ya taifa na tamaduni,” amesema. 
Amesema Serikali itahakikisha inasimamia kuundwa kwa vyombo vitatu katika kutekeleza sheria ya huduma za habari, ambavyo ni baraza huru la habari, Bodi ya Ithibati na kuwepo kwa mfuko wa kusaidia wanahabari.

No comments:

Post a Comment