MAMA MOBETO AFUNGUKA JUU YA KIPIGO KIZITO KWA MWANAE.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 18 May 2018

MAMA MOBETO AFUNGUKA JUU YA KIPIGO KIZITO KWA MWANAE..

DAR ES SALAAM: Mama wa mwanamitindo Hamisa Mobeto, Shufaa Ally amefungukia madai yanayosambaa mitandaoni kuwa mwanaye alipata kipigo kutoka kwa mama wa mzazi mwenziye, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Sandra’.
Juzi Jumanne madai hayo yalisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii huku wakiposti wigi walilodai kuwa ni la Mobeto likiwa limechafuka wakidai eti ni kutokana na kichapo hicho kilichotokea nyumbani kwa mama Diamond, Madale jijini Dar.
Akizungumza  mama Mobeto alisema kuwa hata yeye ameziona habari hizo kwenye mitandao ya kijamii kuwa mwanaye amepigwa na mkwewe huyo lakini ni habari ambazo hazina ukweli wowote. “Unajua mimi nashangaa sana watu wanavyoamini habari za mitandao ambazo hazina ukweli, mimi nikiona huwa haziniumizi kichwa, waache wasema wakichoka watanyamaza,” alisema mama huyo.
Mama huyo aliongeza kuwa Hamisa hawezi kupigwa hata siku moja kwani ni mtu mzima lakini akaongeza kuwa anavyodhani yeye mama Diamond hawezi kufanya kitu kama hicho.
“Hamisa ni mtu mzima, nani wa kumpiga na amefanya kosa gani mpaka apigwe? Hakuna kitu kama hicho na wala sijashtuka kwa sababu ukweli naujua mimi hapa,” alisema mama huyo.

No comments:

Post a Comment