Msanii Harmonize amedai kuwa video ya faragha iliyovuja mtandao ikimuonyesha Diamond akiwa na wanawake wawili ambao miongoni mwao alikuwepo Hamisa Mobetto, ilikuwa ni sehemu ndogo ya movie waliyokuwa waki-shoot.
Harmonize ameiambia Citizen Radio kuwa movie hiyo inalenga kuwafundisha wanaume ambao wamekuwa na tabia za kuwadhalilisha wanawake.
“Walikuwa wanashuti movie ambayo inaelezea wanaume ambao wanadhalilisha wanawake. Sasa ili iweze kuleta attantion, ile iweze kulata item of bisness, iweze kuleta value wakamtumia Diamond kama mtu ambaye ameshaonekana katika mahusiano tofauti tofauti,” amesema Harmonize.
Utakumbuka April 19, 2018 Diamond Platnumz aliomba radhi Watanzania kutokana na kusambaza video hizo, hiyo ilikuwa ni baada ya kuitwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambapo alisema kuwa amejifunza sheria za makosa ya kimtandao na kuhaidi kutorudia tena
No comments:
Post a Comment