Baada ya Zari The Boss Lady kukataa gari aina ya Range Rover Sport ya mwaka 2017 kutoka kwa Ringtone Apoko ambaye ni msanii wa muziki wa Injili nchini Kenya, muimbaji huyo ameibuka na mapya tena.
Katika mahojiano na kipindi cha 10 Over 10 cha Citizen TV, Ringtone Apoko amesema kwa mara ya kwanza aliona taarifa za Zari kuachana na Diamond katika TV lakini kwake ilikuwa ni habari ya kawaida kama zilivyo nyingine.
Hata hivyo anaeleza kuwa alipokwenda kulala alijikuta akikosa usingizi kitu ambacho hakikuwa kawaida kwake.
“Kwa mapenzi ya Mungu kwa dakika chache nikapata usingizi, wakati nimelala nikaota na kuona Zari. Nikaamka nikasikia sauti ikiniambia Zari ndiye mtu sahihi kwangu,” amesema.
Wakati Zari akiwa nchini Kenya kwa ajili ya event yake ‘The Colour Purple’ iliyofanyika weekend iliyopita, alisema hamfahmu kijana huyo kwani ana watu zaidi ya milioni 3.9 katika mtandao wa Instagram ambao wanamfuatilia.
No comments:
Post a Comment