Kwenye ujumbe alioutuma kutoka nchini Dubai ambako bado yupo, Miguna amesema Odinga hakupaswa kula bata na watu waliompokonya urais wake, na yeye alkiyemuapisha kuendelea kupata misuko suko huku akiachwa bila msaada.
"Raila Odinga hawezi na hakupaswa kufurahia Pasaka na kula pamoja na waliomdhulumu, huku mtu aliyemuapisha kuwa Rais wa watu 'akiuawa' na watu hao ambao wamemuibia uchaguzi, kuua na kupoteza wafuasi wake", ameandika Miguna kwenye ujumbe huo alioutuma.
Sambamba na hayo, Miguna ametoa ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter akimsema Gavana Joho wa Mombasa ambaye naye alikuwa mstari wa mbele wakati wa harakati za kuapishwa kwa Odinga, hajawahi kumpigia simu wala kumjulia hali, hata kuzungumza naye jambo lolote.
Miguna amekuwa mtu wa kuondolewa nchini Kenya baada ya kumuapisha Rais Odinga, ambapo mara ya kwanza alipelekwa Canada kwa kuwa ana uraia wa nchi hiyo pia, na hivi sasa kupelekwa Dubai huku akiwa usingizini bila kujitambua, baada ya kumdunga dawa za usingizi.
No comments:
Post a Comment