MESSI KUREKEBISHA REKODI YA ITALY? - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 10 April 2018

MESSI KUREKEBISHA REKODI YA ITALY?

Hadi sasa Messi ameshacheza mechi 9 nchini Italia lakini amefanikiwa kufunga mabao mawili tu katika mechi hizo ambayo aliyafunga Novemba 2011 na Oktoba 2013 dhidi ya AC Milan.
Pia Barcelona inakabiliwa na rekodi ya kutoshinda nyumbani kwa Roma ambapo katika mechi mbili walizokutana Roma imeshinda moja na kutoka sare moja. Roma waliifunga Barcelona mabao 3-0 mwaka 2002.
Katika mechi sita za mwisho ambazo Barcelona wamecheza nchini Italia hawajafanikiwa kushinda ambapo kati ya hizo wametoa sare nne na kufungwa mbili hivyo leo watakuwa na kazi ya kurekebisha rekodi hizo.
Kwa mujibu wa matokeo ya mechi ya kwanza iliyopigwa nchini Hispania wiki iliyopita ni kama Barcelona wameshaweka mguu mmoja nusu fainali, baada ya kufanikiwa kushinda mabao 4-1. Leo wanahitaji sare tu au wasifungwe kuanzia mabao 3-0.

No comments:

Post a Comment