Hii imekuwa ni mara ya kwanza kwa taifa hilo linalojumuisha mataifa kama England, Scotland, Wales na Ireland ya Kaskazini kukosa mwamuzi kwenye fainali za Kombe la dunia ndani ya miaka 80 iliyopita.
FIFA pia imetangaza makamisaa 63 wa michezo lakini hakuna hata kamisaa mmoja kutoka Uingereza. Pia shirikisho hilo linatarajia kutangaza majina ya mwisho ya wataalam wa teknolojia ya Video Assistance Refaree (VAR).
Howard Webb ndio alikuwa mwamuzi wa mwisho kutoka England kuchaguliwa kwenye orodha ya mwamuzi wa fainali za Kombe la Dunia ambapo aliteuliwa kwenye fainali za 2010 nchini Africa Kusini na 2014 nchini Brazil.
Mark Clattenburg alikuwa mwamuzi pekee kutoka Uingereza aliyejumuishwa kwenye orodha ya kwanza iliyotangazwa mwaka 2016 kwaajili ya mchujo wa orodha ya mwisho lakini aliondolewa baada ya mwamuzi huyo kuacha kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment