FAMILIA YA ROMA YAINGIWA NA HOFU KUBWA.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 31 March 2018

FAMILIA YA ROMA YAINGIWA NA HOFU KUBWA..

Mke wa Rappa anaye Fanya vizuri kwenye muziki Bongo Roma Mkatoliki ameonyesha hofu kubwa juu ya mambo ya sanaa anayofanya mume wake na kufikia hatua kuwaza kwa sasa Roma ataimba nn?

Mke wa msanii huyo anayefahamika kwa jina la Nancy ambaye pia ni mama wa watoto wawili wa msanii huyo ameonyesha wasiwasi wake huo kutokana na matatizo yaliyomuandama mume wake huyo ikiwa ni pamoja na kufungiwa kufanya kazi za sana kwa miezi sita ingawa siku ya Ijumaa iliyopita Waziri husika alitangaza kumfulia na kumpatia sharti mija la kujisajili kwenye Baraza la Sanaa Taifa.
Nancy amesema kwamba "Dah nawazaa sijui Baba ataimba nini Sasa 'Round' hii!!!! Nways Tutegee sikio Tu.
Hata hivyo kabla ya kuuhariri ujumbe huo Mke wa  Roma alidai kuwa mumewe anakaziwa kila njia anayojaribu kupenya ambapo amemshauri mumewe kukaa kimya kwani bado anamuhitaji huku akionyesha hofu kwenye wimbo aliouandika jina "NIKIFA CHIMBENI MAKABURI MATATU”.
Roma ni msanii ambaye ni muhanga wa kufungiwa katika kazi zake za sanaa ambapo 2015 alifungiwa wimbo wa 'Viva Roma, na mwaka 2017 mwishoni alifungiwa wimbo wa Kibamia ambao ndiyo uliopelekea kupewa kifungo cha miezi sita.

No comments:

Post a Comment