SIHOFII KUFUNGIWA KIMUZIKI : TIMBULO - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 28 March 2018

SIHOFII KUFUNGIWA KIMUZIKI : TIMBULO

LICHA ya baadhi ya wanamuziki kufungiwa nyimbo zao na serikali kutokana na kuwa kinyume na maadili, msanii wa Bongo Fleva, Ally Timbulo ameeleza kwamba hana hofu na hilo kwani muziki wake ni wa Kiafrika zaidi.
Akistorisha na Risasi Vibes, Timbulo alisema muziki wake una asili ya Kiafrika na siyo asili ya Ulaya kama wanamuziki wengi wanavyofanya ambao wanaacha maungo nyeti wazi au kucheza kihasara hivyo hana hofu kabisa kwamba serikali itamfungia.
“Sina muziki wenye asili ya Ulaya, muziki wangu ni wa Kiafrika, kwa hiyo sina shaka na kufungiwa maana hata video zangu nafanya zenye maadili yanayotakiwa ambapo zinaangaliwa na wakubwa kwa wadogo,” alisema Timbulo.
Hata hivyo aliwataka wasanii wenzake kufuata utaratibu kwani kila mahali kuna utaratibu na sheria zake hivyo inawapasa kuzingatia hilo ili kuweza kusonga mbele zaidi.

1 comment:

  1. Jardin Casino 22Bet Sign In For Sale
    Jardin is a gambling site that offers a virtual sports betting experience as air jordan 18 retro yellow suede to us a way where to order air jordan 18 retro to enjoy a virtual sports betting experience as air jordan 18 retro men to good site a member air jordan 18 retro toro mens sneakers sports of the air jordan 18 retro varsity red shipping

    ReplyDelete