ROMA MKATOLIKI NAYE ALIA NA KIFUNGO CHA WAZIRI SHONZA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday 21 March 2018

ROMA MKATOLIKI NAYE ALIA NA KIFUNGO CHA WAZIRI SHONZA.

 Sikuchache baada yaNaibu Waziri wa Habari Sanaa, Michezo na Utamaduni, Juliana Shonza kusema wasanii waliofungiwa nyimbo zao wanatakiwa kufuata taratibu kama wana malalamiko, msanii wa Bongo Fleva, Ibrahim Musa maarufu  Roma Mkatoliki amesema alifuata taratibu hizo lakini amegonga mwamba.
Roma ameyasemahayoleo Jumatano Machi21,2018 katikamahojiano nakipindi cha XXL kinachorushwa nakituo cha Radio Clouds, akidai kuwa adhabu yakufungiwamiezi sita inamuumiza nakuomba apunguziwe au kutozwa faini ili yaishe.
Machi1, 2018 Shonza alimfungia Roma Mkatoliki kutojihusisha natasniaya muziki kwa kipindi cha miezi sita nakwamba msanii huyo alipopewa muda wa kurekebisha wimbo wake wa Kibamia, ameshindwa kutekeleza agizo hilo.
Katika kipindi hicho, Roma amesema tangusiku alipofungiwa alijitahidi kufanya taratibu za kumuona naibu wazirihuyo kama ambavyo alitaka, ikiwemo kufunga safari hadi ofisinikwake lakini hakufanikiwa.
Amebainisha kuwa amefungiwa wakati tayari ana shoo za kufanya naalishachukua fedha, ikiwemo shoo yaKili Marathon ambayo baadaye alitakiwa kurejesha fedha hizo.
“Shoo yaKili Marathon mimi naStamina kupitiakundi letula Rostam tulikuwa tumelipwa vizuri, lakinijuhudi za kufanikisha ziligonga mwamba hata kwa kuomba barua kidogo ya utambulisho.Mambo kama haya yanatuharibia kuaminika tena kwa kampuniambazo zinatupa kazi,” amesema.
Kuhusukumuona naibu waziri amesema, “Siku moja nilitoka hospitali nikampitia rafiki yangu Madee na Askofu nikawaambia twendeni tukamuone mheshimiwalakini mimisikupewa ruhusaya kumuona. Wengine wote walipewa ruhusa, basi nikawatuma waowafikishe ujumbe kwa sababu niliogopa kulazimisha kwa kuwa ningeonekana nafanya fujo.”
Amesema alitakiwa kupewa muda kabla yahatua iliyochukuliwa kuliko kudhaniwa kuwa anakaidi agizo la kutakiwa kuripoti ofisiza Baraza laSanaa la Taifa (Basata).
“Walitakiwa kujua kuwa nilikuwana udhuru napia hiyo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza,” amesema na kubainisha kuwa hata kama alipigiwa simu, aliogopa kupokea kwa sababu yauoga alionao tangualipotekwa na watu wasiojulikana mwaka jana.
“Inaonekana Roma hajafanya kitu chochote tangulitokee jambo hilo lakiniambacho mimi sijafanya ni kujakwenye media kusema leo nimeandika barua au vipi? Sikupewa barua kwa wakati ule nilipewaujumbe tena kwa namba ngeni.”

No comments:

Post a Comment