MWANAMUZIKI wa kike anayefanya poa na ngoma yake ya Homa, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amefunguka kuwa kwa sasa muziki umerudi kwenye mfumo wa albamu kama zamani hivyo yupo kwenye mata-yarisho ya albamu yake mpya ambayo atawa-shirikisha wanamuziki mbalimbali akiwemo Cardi B, kutoka Marekani.
Akichonga na Risasi Vibes, Lulu Divaalisema muziki umehamia kwenye albamu na ni heshima pia kufanya kazi nzuri ambayo hata baadaye inabaki kwenye historia hivyo kumshirikisha Cardi B ni chachu ya kutangaza muziki wake kimataifa zaidi.
“Najiandaa kufanya albamu kama ambavyo wanamuziki wakubwa wamekuwa wakifanya hivi karibuni na albamu yangu itakuwa imesheheni wanamuziki wakali ndani na nje ya Afrika na ndani yake nitamshirikisha Cardi B, kutoka Marekani, nafurahi sana maana naona nikitoka kimataifa zaidi kwa kweli,” alisema Lulu Diva.
No comments:
Post a Comment