Kumbe Jezi ya Banda ni dili ! - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday 4 March 2018

Kumbe Jezi ya Banda ni dili !


ACHANA na sare ya 1-1 waliyopata usiku wa kuamkia jana na kuifanya timu yao ya Baroka FC dhidi ya Bidvest Wits bna kushuka nafasi moja hadi ya saba kutokana na ushindi wa Cape Town City dhidi ya Chippa United, jezi ya Abdi Banda sio mchezo.
Unaambinwa thamani ya jezi ya beki huyo wa kimataifa wa Tanzania anayoivaa ndani ya klabu ya Baroka inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini ni zaidi ya jezi za mastaa wa Simba na Yanga.
Ndio, jezi moja ya Banda ni R400.00 ya Afrika Kusini (sawa na Sh. 75,740) ambapo kiwango hicho cha fedha unaweza kutumia kununua jezi ya Simba, Yanga na bado chenji ikabaki. Jezi moja ya klabu za Simba na Yanga ni kati ya Sh. 15,000-20,000.
Baroka ya Banda imekuwa na utamaduni wa kuuza jezi zake kama njia moja wapo ya kujiingizia kipato ukiachilia mbali vyanzo vingine walivyonavyo.
Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Ga-Mphahlele karibu na mji wa Polokwane, Banda alisema ni ngumu kujua kwa haraka haraka mauzo ya jezi zake zimefikia ngapi tangu ajiunge na timu hiyo, lakini zinauzika sana kwa mashabiki.
“Ofisi imekuwa ikihusika na hayo mambo na wao ndiyo wanaweza kuwa na idadi kamili ila binafsi ningumu kusemea hilo,” alisema Banda.
Mbali na thamani ya jezi ya beki huyo wa zamani wa Simba, Banda ambaye juzi alicheza dakika zote 90 wakati Baroka ikitoshana nguvu ya bao 1-1 na Bidvest Wits.
Katika mchezo huo, Banda alifanya kazi kubwa ya kumzuia straika hatari Bidvest, Lehlohonolo Majoro mwenye mabao sita.
“Huyo jamaa nilicheza naye man to man japo kuna muda nilikuwa nikibadilishana na mwenzangu kwenye kuwazuia washambuliaji wao, aliyefunga bao lao kama ulimuona alikuwa ni winga,” alisema Banda.
Baroka itacheza tena Jumamosi ijayo dhidi ya Steenberg United kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA nchini humo maarufu kama South Africa Cup.

No comments:

Post a Comment