Davido aanguka jukwaani akipanda kwa mbwembwe... - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 4 March 2018

Davido aanguka jukwaani akipanda kwa mbwembwe...

Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria, Davido amejikuta akipoteza mzuka baada ya kujikwaa wakati akipanda kwa mbwembwe jukwaani tayari kwa kutumbuiza nchini Rwanda.

Davido ambaye alikuwa anaonekana kama tayari ameshapata ulabu ilimchukua sekunde kama 30 kukaa kimya jukwaani akivalishwa tena phone masikioni ambazo zilikatika alipojikwaa wakati akipanda jukwaani.

Hata hivyo, baada ya ajali hiyo ndogo Davido aliendelea kutumbuiza ambapo maelfu ya watu walihudhuria kwenye show hiyo ambayo ipo kwenye ziara ya Davido ijulikanayo kwa jina la  “30 billion africa tour 2018”  iliyofanyika kwenye uwanja wa mpira wa taifa wa Amahoro.

Akiwa nchini Rwanda, Davido ametoa msaada wa dola $5,000 sawa na Tsh milioni 11.2 kwenye shule ya muziki nchini Rwanda

No comments:

Post a Comment