JUX AFUNGUKA KUTAMANI KUWA NA MTOTO. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 28 March 2018

JUX AFUNGUKA KUTAMANI KUWA NA MTOTO.

Msanii wa RnB Jux amesema anatamani kupata mtoto na Mungu akijali hivi karibuni atafanikisha hilo.

Muimbaji huyo ambaye amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Vanessa Mdee kwa muda sasa, amekiambia kipindi cha Uhondo, E Fm kuwa kulingana na umri wake wa miaka 28 anatarajia hadi atakapofikisha 30 atakuwa na mtoto.

“Yeah sina mtoto lakini Mwenyenzi Mungu akipenda siwezi nikasema siku gani lakini soon tu, Mwenyenzi Mungu akinijalia ninavyotaka mimi itakuwa (na mtoto) lakini ni kitu natamani sana kuwa nacho,” amesema.

“Sio kuzaa tu mtoto, je unazaa na nani na huyu mtu unazaa naye yeye mwenyewe yupo vipi, siwezi nikawa na mtoto na msichana yeyote kwanza, japo sometime huwa inatokea ila nakuwa makini sana sana,” amesema.

Inafahamika fika mpenzi wa Jux ni muimbaji Vanessa Mdee ambaye siku za hivi karibuni zilizuka taarifa kuwa ni mjamzito, hata hivyo Vanessa alikanusha taarifa hizo kwa kueleza kuwa hazikuwa na ukweli wowote. Jux kwa sasa anafanya vizuri ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Fimbo.

No comments:

Post a Comment